Watu takriban milioni 733 walikabiliwa na njaa 2023: UN Ripoti SOFI

5 months ago 128

Ripoti hiyo ya kila mwaka iliyozinduliwa nchini Brazili katika mkutano wa mawaziri wa nchi 20 zenye kipato cha juu duniani  au G-20 imeonya kwamba  dunia iko mbali sana kufikia lengo la 2 la Maendeleo Endelevu, la kutokomeza njaa, ifikapo mwaka 2030.

Pia inafichua kwamba dunia imerudi nyuma miaka 15, huku viwango vya utapiamlo vikilinganishwa na vile vya mwaka  2008-2009.

Ripoti inasema licha ya maendeleo kiasi yaliyopigwa katika maeneo maalum kama vile kudumaa na kunyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee, viwango vya njaa duniani vimedorora kwa miaka mitatu mfululizo, na mwaka 2023, kulikuwa na watu milioni 152 zaidi wenye utapiamlo kuliko mwaka 2019.

Kuliko na changamoto kubwa

Kwa mmujibu wa mashirika matano ya Umoja wa Mataifa yaliyoandaa ripoti hiyo lile la chakula na kilimo FAO, la mpangowa chakula duniani WFP, la ufadhili wa maendeleo ya kilimo IFAD, la kuhudumia  watoto UNICEF na la afya duniani WHO bara linaloongoza kwa ongezeko la watu wenye njaa ni Afrika kwa asilimia  20.4, Asia  asilimia 8.1 ingawa bado ni changamoto kubwa, kwani eneo hilo ni nyumbani kwa zaidi ya nusu ya watu wenye njaa duniani na Amerika ya Kusini inaonyesha hatua ya matumaini kiasi ikiwa na asilimia 6.2.

Ripoti imeongeza kuwa kuanzia 2022 hadi 2023, njaa iliongezeka katika maeneo ya Asia Magharibi, Karibea, na maeneo mengi ya Afrika.

Na imeonya kwamba ikiwa hali ya sasa itaendelea, takriban watu milioni 582 watakuwa na utapiamlo sugu ifikapo 2030, nusu yao wakiwa barani Afrika.

Masuala muhimu zaidi ya njaa

Ripoti hiyo imegawanyika katika sehemu tatu: Mosi viasharia vya njaa ambapo inasema upatikanaji wa chakula unaendelea kuwa mtihani kwa mamilioni ya watu,

Mwaka 2023, karibu watu milioni 2330 ulimwenguni walikabiliwa na uhaba wa chakula wa wastani au mbaya.

Miongoni mwao, zaidi ya wsatu  milioni 864 walikumbwa na uhaba mkubwa wa chakula, wakati mwingine wakienda siku nzima au zaidi bila kula.

ukosefu wa fursa za kiuchumi za kupata mlo kamili ni changmoto kubwa , inaathiri zaidi ya theluthi moja ya watu duniani.

Kwa takwimu mpya kuhusu bei za vyakula, unaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 2800 hawakuweza kumudu lishe bora mwaka 2022.

Tofauti hii inaonekana zaidi katika nchi za kipato cha chini, ambapo asilimia 71.5 ya watu hawawezi kumudu lishe bora, ikilinganishwa na asilimia 6.3 katika nchi zenye kipato cha juu.

watoto kuzaliwa na uzito mdogo na kudumaa ni matatizo sugu karibu asilimia 15, na udumavu miongoni mwa watoto wa chini ya umri wa miaka mitano, ingawa umepungua hadi asilimia 22.3, bado haufikii malengo.

Aidha, matukio ya  uzito mdogo wa kupindukia kati ya watoto hayajaona maboresho makubwa, wakati upungufu wa damu kati ya wanawake wenye umri wa miaka 15-49 umeongezeka.

na katika muongo uliopita kumekuwa na ongezeko kubwa  la utipwatipwa. kutoka asilimia 12.1 mwaka  2012 hadi asilimia 15.8 mwaka 2022.

Makadirio yanaonyesha kuwa ifikapo mwaka 2030 kutakuwa na zaidi ya watu wazima milioni 1200 tipwatipwa duniani.

Mfumuko wa bei, vita na mabadiliko ya tabianchi ndiochachu

Pili: imetaja sababu za ongezeko la njaa kuwa ni  mfumuko wa bei, vita na mabadiliko ya tabianchi.

Ripoti inasema mienendo hii inaangazia changamoto za utapiamlo katika aina zake zote na hitaji la dharura la afua zinazolengwa, kwani ulimwengu hauko kwenye njia ya kufikia malengo yoyote kati ya saba ya lishe ya kimataifa ifikapo mwaka 2030.

Ukosefu wa uhakika wa chakula na utapiamlo unazidi kuwa mbaya kutokana na mchanganyiko wa mambo, kama vile mfumuko wa bei wa vyakula unaoendelea, ambao unaendelea kufifisha faida za kiuchumi za idadi kubwa ya watu katika nchi nyingi.

Sababu kuu kama vile migogoro, mabadiliko ya tabianchi na kuzorota kwa uchumi vinazidi kkuongezeka mara kwa mara.

Matatizo haya, pamoja na vipengele vya msingi kama vile vyakula vyenye afya visivyoweza kumudu kutokana na bei, mazingira ya chakula yasiyofaa, na ukosefu wa usawa unaoendelea, sasa yanapatana kwa wakati mmoja, na kuongeza athari zake.

Mfano wa kuingwa

Kwa upande wa Amerika ya Kusini, mwanauchumi mkuu wa FAO amesisitiza kuwa eneo hilo ni mfano wa kuigwa na dunia nzima kutokana na uwekezaji wake katika mipango ya hifadhi ya jamii hususan Amerika Kusini.

"Brazil, Colombia, Peru na Chile zina mifumo dhabiti ya hifadhi ya jamii. Mifumo hii inawaruhusu kuguswa haraka na mabadiliko na kulenga rasilimali za kifedha zinazopatikana kwao," amesema Máximo Torero.

Mtaalamu huyo ameeleza kuwa, kwa kuwa na ufanisi katika mbinu zao, nchi hizi zinaweza kuzingatia idadi ya watu walio hatarini zaidi.

Kwa kuongezea,amesema eneo hilo limejikwamua haraka kutoka kwa janga la coronavirus">COVID-19 ikilinganishwa na sehemu zingine za ulimwengu, na zaidi ya watu milioni tano wameondolewa kwenye njaa katika miaka mitatu iliyopita.

Ufadhili wa kumaliza njaa

Na tatu nini kifanyike: Ripoti inapendekeza uwekezaji ili kufadhili kukomesha njaa, uhaba wa chakula na aina zote za utapiamlo.

Mada kuu ya ripoti ya mwaka huu ni uwekezaji. Ufadhili wa Kukomesha Njaa, ukosefu wa chakula na aina zote za utapiamlo, inasisitiza kwamba kufikia lengo la kutokuwa na njaa kabisa kunahitaji mbinu ambayo inajumuisha kubadilisha na kuimarisha mifumo ya chakula cha kilimo, kukabiliana na ukosefu wa usawa na kuhakikisha lishe yenye afya nafuu na inayopatikana kwa wote. Ili kufanya hivyo, inahitaji ufadhili mkubwa na wa faida zaidi.

"Imeonekana kuwa njia ya haraka ya kuondokana na njaa na umaskini ni uwekezaji katika kilimo katika maeneo ya vijijini. Lakini hali ya kimataifa na kifedha imekuwa ngumu zaidi tangu Malengo ya Maendeleo Endelevu yalipopitishwa mwaka 2015. Kukomesha njaa na utapiamlo kunatuhitaji. kuwekeza zaidi, na werevu zaidi," amesema Rais wa IFAD Alvaro Lario.

Mkurugenzi Mtendaji wa WFP ametoa wito kwa viongozi wa G20 "kufuata mfano wa Brazil na kuweka kipaumbele katika hatua kabambe ya kimataifa dhidi ya njaa na umaskini."

Cindy McCain ameongeza kuwa "Tuna teknolojia na ujuzi wa kumaliza uhaba wa chakula, lakini tunahitaji fedha kwa haraka ili kuwekeza kwa kiwango kikubwa." 

Source : UN Habari

SHARE THIS POST