Watatu wafungiwa leseni ya magari , akiwemo kada wa chadema 

2 months ago 289

KADA wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anayeshitakiwa kwa kosa ka kusambaza taarifa za uongo kwenye mtandao wa X kuwa ameshambuliwa na watu wasiojulikana mjini Iringa, Vitus Nkuna (29) amefungiwa leseni ya udereva kwa miezi sita.

 

Akizungumza na wanahabari leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi amesema adhabu hiyo inayomtaka pia kulipa faini imeanza Oktoba 7, mwaka huu.

 

Amesema Nkuna amepewa adhabu hiyo kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na kusababisha ajali akiwa anaendesha gari yenye namba za usajili T797 DYC aina ya Volkswagen na kugonga gari yenye namba T975 EDC aina ya Toyota Probox katika tukio lililotokea Septemba 30, 2024.

 

“Tulimkamata Nkuna kwa makosa mawili, moja ni kusababisha ajali ambalo hukumu yake ndio hiyo ya kufunguwa leseni na kosa la pili ambalo shauri lake linaendelea mahakamani ni kutoa taarifa hizo za uongo katika mtandao wa X,” amesema.

Source : Millardayo.com

SHARE THIS POST