Walibya 95 wakamatwa katika shamba linaloshukiwa kuwa kambi ya jeshi Afrika Kusini

3 months ago 58

Uvamizi huo ulifanyika asubuhi na mapema, karibu na mji wa White River, katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Mpumalanga, takriban kilometa 360 Mashariki mwa Johannesburg, wamesema.

“Mahali hapo, ambapo awali palitengwa kuwa eneo la mafunzo, panaonekana kubadilishwa kuwa kambi haramu ya jeshi “ taarifa ya polisi ilisema.

“Watu 95 waliowekwa chini ya ulinzi ni raia ya Libya na kwa sasa wanahojiwa na mamlaka husika.”

Picha za televisheni za Newzroom Afrika kutoka eneo la tukio zilionyesha polisi wengi walikuwepo katika kambi hiyo inayoshukiwa, inayojumuisha uwepo wa mahema ya kijeshi na mifuko ya mchanga.

Picha hizo zimeonyesha wanaume waliowekwa chini ya ulinzi wakiwa wamesimama katika makundi na wamevaa nguo za kiraia.

Waziri wa ulinzi na usalama wa Mpumalanga, Jackie Macie ameliambia shirika la habari la eneo hilo, wanaume hao waliingia nchini mwezi April na kudai wanapatia mafunzo ya kuwa walinzi.

Pia kuna wasiwasi kuwa nchi hiyo inaweza ikawa kituo cha ufadhili wa wanajihadi barani Afrika.

Source : VOA Swahili

SHARE THIS POST