Wakaazi wa Florida nchini Marekani watathmini uharibifu wa mali zao

3 months ago 155

Watu wasiopungua 10 wamekufa na waokoaji walikuwa bado wanawaokoa watu kutoka kwenye mito iliyofurika.

Wakazi wa Florida waliokwama katika mitaa iliyojaa maji, walikusanya vifusi ili kutathmini uharibifu wa nyumba zao siku ya Ijumaa baada ya kimbunga Milton kuleta athari kwenye jamii za pwani na kusababisha madhara.

Watu wasiopungua 10 wamekufa na waokoaji walikuwa bado wanawaokoa watu kutoka kwenye mito iliyofurika, lakini wengi walionyesha faraja kwamba Milton hakikuwa kimbunga kibaya zaidi.

Kimbunga hicho kilipiga Tampa eneo lenye watu wengi, na kuwepo dhoruba ya kutisha ambayo wanasayansi waliogopa hali ambayo haijawahi kutokea. Gavana Ron DeSantis aliwaonya watu kutowaangusha walinzi wao, hata hivyo akielezea vitisho vya usalama vinavyoendelea ikiwa ni pamoja na nyaya za umeme zilizoanguka, na maji yaliyosimama ambayo yanaweza kuficha vitu hatari.

Source : VOA Swahili

SHARE THIS POST