Mkuu wa zamani wa kitengo cha ujasusi aliwasilisha malalamiko ya jinai dhidi ya Ramaphosa kufuatia wizi katika shamba lake la la Phala Phala kaskazini mashariki mwa jimbo la Limpopo, akidai kuwa rais alifanya makosa kwa kujaribu kuficha wizi wa dola milioni 4 taslimu.
Kufuatia uchunguzi wa kitengo maalum cha polisi, mwendesha mashataka wa Limpopo “amechukua uamuzi wa kutomshtaki mtu yeyote”, mamlaka ilisema katika taarifa.
“Amebaini kuwa hakuna matarajio ya msingi ya kufungua mashtaka kulingana na ushahidi uliomo katika kesi hiyo.”
Mamalamiko hayo yalidai Ramaphosa alihusika katika utakatishaji wa fedha na ufisadi kuhusiana na wizi huo, taarifa hiyo ilisema.