Virusi vya Marburg nchini Rwanda vimekwisha

5 days ago 107

Rwanda imesema mlipuko wa virusi hatari vya Marburg nchini humo umekwisha, na hakuna maambukizi mapya kwa takriban wiki mbili.

Mlipuko wa Marburg ulitangazwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa Septemba 2024 na Rwanda ilianza kutoa chanjo dhidi ya Marburg mwezi Oktoba.

“Tangu wakati huo tumekuwa tukipambana na virusi hivi ili kuhakikisha kuwa vimedhibitiwa nchini Rwanda,” Waziri wa Afya Sabin Nsanzimana aliwaambia waandishi wa Shirika la Umoja wa Afrika la Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika CDC.

“Nina furaha sana kuripoti leo kwamba imepita karibu wiki mbili bila maambukizi mapya na mwezi bila kifo kinachohusiana na ugonjwa wa Marburg,” alisema.

“Virusi vya Marburg nchini Rwanda vimekwisha,” aliongezea.

“Wagonjwa wote wanaotibiwa virusi hivi wanaruhusiwa kuondoka … tunapiga hatua nzuri sana.”
Mkuu wa Afrika CDC barani Afrika Jean Kaseya alikuwa amesema mwezi Oktoba kwamba virusi hivyo vimedhibitiwa.

Source : Millardayo.com

SHARE THIS POST