Viongozi wa Misri, Eritrea na Somalia waahidi kushirikiana kudumisha usalama Katika Pembe ya Afrika

1 week ago 13

Viongozi wa Misri, Eritrea na Somalia Alhamisi waliahidi kushirikiana pamoja juu ya usalama wa kikanda katika mkutano usio wa kawaida uliofanyika licha ya mivutano inayozidi kuongezeka katika Pembe ya Afrika.

Wasiwasi kuhusu utulivu katika eneo hilo lenye usalama mdogo umeongezeka kutokana na vita nchini Sudan, makubaliano yenye utata kati ya Ethiopia na jimbo lililojitenga la Somaliland, na hali katika Bahari ya Sham, ambako waasi wa Kihouthi wa Yemen wamefanya mashambulizi mengi dhidi ya meli za biashara.

Mkutano wa Alhamisi mjini Asmara umeashiria kuimarishwa kwa ushirika mpya wa kikanda katika Pembe ya Afrika, huku Ethiopia, ikitengwa katika ushirika huo.

Uhusiano umezorota vibaya kati ya Ethiopia na jirani yake Somalia, ambayo ilikasirishwa na makubaliano ya bahari na Somaliland na tangu wakati huo Somalia imekuwa na ushirikiano wa karibu na Cairo, hasimu wa Addis Ababa.

Mkutano huo wa siku tatu mjini Asmara uliitishwa na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki na umewashirikisha wenzake wa Misri Abdel Fattah al-Sisi na Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia.

Source : VOA Swahili

SHARE THIS POST