UN Ripoti: Kupungua kwa kiasi cha wadudu kunatishia mustakbali wa ndege wanaohama

3 months ago 71

Katika maadhimisho haya ya pili ya kila mwaka ya Siku ya Ndege Wanaohama Duniani ambayo huwa kila mwaka tarehe 12 Oktoba, kampeni ya kimataifa, iliyoandaliwa na mtandao wa washirika wa kimataifa, inataka hatua za haraka na endelevu ili kuwalinda ndege wanaohama na wadudu wanaowategemea ili kuendelea kuishi.

Kauli mbiu ya mwaka huu, ni "Linda Wadudu, Linda Ndege", na inasisitiza jukumu muhimu la wadudu katika mzunguko wa maisha wa ndege wengi wanaohama na inamulika kushuka kwa kiwango cha kutisha kwa idadi ya wadudu ulimwenguni.

Mkataba wa Uhifadhi wa viumbe wanaohama wa wanyama wa porini (CMS), mkataba wa viumbe hai wa Umoja wa Mataifa na mmoja wa washirika wakuu wa kampeni ya Siku ya Ndege Wanaohama Dunia ulitayarisha utafiti wa kwanza wa aina yake kuhusu kupungua kwa wadudu na umuhimu wake kwa aina za ndege zinazohama, ambao uliwasilishwa katika Kikao chake cha Kumi na Nne cha Mkutano wa Wanachama (COP14) huko Samarkand, Uzbekistan.

Ndege wanaohama

Ndege wanaohama

Kupungua kwa wadudu na tishio lake kwa wanyama wanaohama

Utafiti huo unasema kwa ndege wanaohama wamegundua kuwa kupungua kwa wadudu kunachangia upotezaji wa idadi ya aina nyingi za ndege wanaohama  ambao wanakula wadudu haswa wale wanaotegemea  wadudu kama chanzo chao kikuu cha chakula.

Wadudu ni muhimu kwa maisha ya sio tu ndege wanaohama duniani kote, lakini pia popo na samaki. Kupungua kwao kunaweza pia kuwa na athari zisizo za moja kwa moja kwa kubadilisha utendakazi wa mfumo wa ikolojia na makazi ndani yake kama vile kubadilisha mimea, ambayo inaweza kutoa ulinzi mdogo kwa aina mbalimbali zinazozalishwa ardhini, au kutoa matunda machache yaliyochavushwa na wadudu kwa ndege wanaokula matunda.

Kwa mujiu wa ripoti ya utafiti huo ya Umoja wa Mataifa "Licha ya kutofautiana kwa ukubwa katika mifumo ya ikolojia na maeneo, ushahidi wa kisayansi umeonyesha kwamba bila shaka, tunakabiliwa na kupungua kwa wadudu duniani kote. Hii inaweza kupimwa kwa mfano kama hasara katika jumla ya majani ya wadudu au utajiri wa aina za viumbe kwa wakati,” amesema Dkt. David Ott kutoka Taasisi ya Ujerumani ya Leibniz ya Uchambuzi wa Mabadiliko ya Biyoanuwai (LIB) na mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo.

Ameongeza kuwa “Ili kukabiliana na athari za kupungua kwa wadudu, tunahitaji kuelewa kwamba aina mbalimbali ni sehemu ya jamii tata, zilizounganishwa, na kwamba bayoanuwai ni muhimu kwa mifumo ya ikolojia kufanya kazi ipasavyo na kutoa huduma kwa wanadamu. Sababu za kupungua kwa wadudu pia hazijatenganishwa, lakini ni mchanganyiko wa mambo kadhaa yaliyounganishwa".

Ndege wahamaji wakiwa katika safari zao kuelekea kusini.

Ndege wahamaji wakiwa katika safari zao kuelekea kusini.

Matokeo muhimu ya ripoti ya CMS ni pamoja na:

• Kupungua kwa majani ya wadudu, wingi, na utofauti kunaleta tishio kubwa kwa spishi zinazohama wadudu, kupunguza upatikanaji wa chakula wakati wa uhamaji na hatua nyingine za mzunguko wa maisha yao, na kuhatarisha spishi nyingi zinazofuatiliwa na CMS.

• Mabadiliko ya matumizi ya ardhi, mabadiliko ya tabianchi, na uchafuzi wa mazingira ni vichochezi vikuu vya kupungua kwa wadudu duniani kote na vichochezi hivi mara nyingi huunganishwa na vinaweza kuchukua hatua kwa wakati mmoja.

• Wadudu na aina mbalimbali za Ndege wanaohama wanaokula wadudu ni muhimu kwa utendaji kazi wa mfumo wa ikolojia na kutoa huduma muhimu za mfumo wa ikolojia, kama vile uchavushaji.

• Bado kuna mapungufu katika kuelewa athari za kupungua kwa wadudu kwa aina za Ndege wanaohama na taarifa zaidi zinahitajika kuhusu hali ya idadi ya watu na mienendo ya idadi ya aina za Ndege wahamao na pia popo haswa.

Source : UN Habari

SHARE THIS POST