UHABA WA MAJI DAR ES SALAAM CHALAMILA ATOA TAMKO ASEMA...

1 month ago 9


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema hatua za haraka zimechukuliwa kukabiliana na uhaba wa maji, ikiwemo kununua mitambo maalumu kwa ajili ya uchujaji na usafirishaji wa maji kutoka kwenye vyanzo vya maji. Ameeleza kuwa hatua hiyo itagharimu Sh6 bilioni, fedha ambazo tayari zimeidhinishwa, na kazi hiyo inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi. Akizungumza leo Jumatano, Oktoba 2, 2024, jijini Dar es Salaam, Chalamila amesema mahitaji ya maji kwa jiji hilo ni lita 685 milioni kwa siku, kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na uzalishaji wa sasa. Ameongeza kuwa uhaba wa maji ni changamoto ya muda mfupi, huku serikali ikijipanga kuleta mitambo itakayosaidia kupunguza tatizo hilo au kulimaliza kabisa.
Source : Mwananchi Digital

SHARE THIS POST