Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Kevin de Bruyne kutua Inter Miami ya Messi? - BBC News Swahili

5 days ago 82

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Kevin de Bruyne kutua Inter Miami ya Messi?

N

Chanzo cha picha, Getty Images

14 Aprili 2025, 05:49 EAT

Inter Miami wana nia kubwa ya kumsajili Kevin de Bruyne kwa uhamisho wa bure mara atakapoondoka Manchester City mwishoni mwa msimu huu. Hata hivyo, mazungumzo bado hayajafikia hatua zozote. (Florian Plettenberg)

Klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia inaweza kufanya usajili wa winga wa Liverpool na Colombia, Luis Diaz, mwenye umri wa miaka 28, kama mbadala wa mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil, Vinicius Jr. (Talksport)

Everton ni klabu ya hivi karibuni kujiunga na mbio za kumnasa mshambuliaji wa England chini ya miaka 21, Liam Delap, 22, kutoka Ipswich Town. (The Sun)

A

Chanzo cha picha, Getty Images

Newcastle wanavutiwa na kiungo wa kati wa Racing Genk na timu ya taifa ya Ugiriki, Konstantinos Karetsas, mwenye umri wa miaka 17, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Bayern Munich, Napoli na vilabu vingine kadhaa vya Premier League. (The Sun)

Wakati huo huo, Newcastle wametuma wafuatiliaji vipaji wake kumtazama kipa wa kimataifa wa Ivory Coast, Yahia Fofana, 24, anayekipiga katika klabu ya Angers nchini Ufaransa, wakijiandaa kuimarisha safu yao ya makipa. (Football Insider)

Arsenal bado wanaonyesha nia ya kumsajili beki wa kimataifa wa Uholanzi kutoka Ajax, Jorrel Hato, mwenye umri wa miaka 19, msimu huu wa joto, ingawa uhamisho wowote unategemea mustakabali wa Jakub Kiwior. (Mirror)

C

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati huo huo, Arsenal hawana mipango ya kumsaini kwa mkataba wa kudumu winga wa Chelsea na timu ya taifa ya England, Raheem Sterling, 30, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo. (Football Insider)

Chelsea na Bournemouth wako tayari kulipa euro milioni 35 (£30.3m) kumsajili kiungo wa Kimarekani Johnny Cardoso, 23, kutoka klabu ya Real Betis ya Hispania. (Fichajes)

Source : BBC Swahili

SHARE THIS POST