Russia imesema imetungua ndege 47 za Ukraine

2 months ago 127

Mkuu wa wafanyakazi nchini Ukraine pia alisema vikosi vya Kyiv vimeshambulia ghala ya mafuta usiku wa kuamkia leo huko mashariki mwa  Russia.

Russia imesema Jumamosi kuwa imetungua ndege 47 za Ukraine zisizokuwa na rubani, huku Kyiv ikiripoti kwamba ilizuia drone 24 zilizorushwa na Russia.

Jeshi la anga la Ukraine limesema makombora mengi yalifyatuliwa kutoka mkoa wa mpakani mwa Russia wa Belgorod, bila kutaja idadi au aina ya makombora hayo. Ilisema Russia ilirusha ndege 28 zisizokuwa na rubani nchini Ukraine, kati ya hizo 24 ziliharibiwa katika mikoa ya Sumy, Poltava, Dnipropetrovsk, Mikolayev na Kherson.

Mkuu wa wafanyakazi nchini Ukraine pia alisema vikosi vya Kyiv vimeshambulia ghala ya mafuta usiku wa kuamkia leo huko mashariki mwa Russia katika mkoa wa Lugansk unaokaliwa na Russia na kuchoma moto ghala. Halikutoa maelezo zaidi.

Source : VOA Swahili

SHARE THIS POST