Ruge: Hatuwezi kukaa kwenye chama ambacho watu hawataki kusikiliza wengine | DW Kiswahili
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, kinaonekana kuingia kwenye mtikisiko mkubwa wa ndani wakati huu viongozi wakuu wa chama hicho wakiendelea kufanya mikutano ya nchi nzima kuhamasisha kile wanachokiita kampeni ya kuzuwia uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, 2025 endapo hakutakuwa na mabadiliko ya kimsingi kwenye sheria, kanuni na mwenendo wa uchaguzi wenyewe. Mohammed Khelef amezungumza na Catherine Ruge, ambaye ni miongoni mwa wanachama wanaopingana na msimamo wa chama chao. Sikiliza #kinagaubaga