MKUU wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Zuwena Omary na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva leo Oktoba 12, 2024 wameungana na wakazi wa mtaa wa Mtanda Juu Manispaa ya Lindi kujiandikisha katika orodha ya daftari la wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za mitaa. Katika zoezi hilo viongozi hao wamehimiza wananchi kujitokeza kujiandikisha waweze kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bora watakaosikiliza na kuzipatia ufumbuzi changamoto zao pamoja na kusimamia vizuri miradi ya maendeleo pindi inapopelekwa kwenye mitaa yao. Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchgaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Juma Mnwele manispaa hiyo inajumla ya vituo vya kujiandikisha 353 na tangu kuanza kwa zoezi hilo jana Oktoba 10 wameandikisha wakazi 68000 na matarajio ya kuandikisha watu 111, 800. “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi “