Nyota wa West Ham ahusishwa na kuhamia Saudi Arabia

1 month ago 205

Mshambulizi wa West Ham United, Mohammed Kudus amehusishwa na kutaka kuondoka katika klabu hiyo, na inaonekana huenda akawa njiani kuelekea Mashariki ya Kati.

Kulingana na Fichajes, vilabu vya Saudi Arabia vina hamu ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Ghana mwenye umri wa miaka 24 na kuondoka kwake itakuwa pigo kubwa kwa The Hammers.

Hakika ni mmoja wa wachezaji bora katika klabu hivi sasa, na West Ham hawawezi kumudu kumpoteza. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa mchezaji muhimu wa West Ham tangu ajiunge na klabu hiyo na uwezo wake wa kufumania nyavu na kutengeneza nafasi za mabao kwa wachezaji wenzake unamfanya kuwa mtaji wa thamani.

Zaidi ya hayo, ana uwezo wa kutosha kufanya kazi katika majukumu mengi ya kushambulia pia

Source : Millardayo.com

SHARE THIS POST