'Nimesaidia kuokoa nyoka 6000 katika miaka 10'

4 months ago 89


Vedhapriya Ganesan ni miongoni mwa wanawake wachache wanaosaidia na kuokoa nyoka katika jiji la India la Chennai na kuwapeleka katika msitu wa hifadhi. Anafanya kazi hiyo ili kupunguza migogoro ya nyoka na binadamu katika maeneo ya mijini. Kwa sababu ya misitu na mito mingi iliyoko Chennai, nyoka wamekuwa wengi na mara nyingi huingia katika maeneo ya makazi wakati wa msimu wa masika. Ganesan amechaguliwa na serikali ya eneo hilo kufanya kazi na maafisa kuwaokoa nyoka hao na kuwaachilia katika misitu ya hifadhi. Anasema ameisaidia timu yake kuokoa zaidi ya nyoka 6000 katika kipindi cha miaka 10 iliyopita #bbcswahili #india #wanyama Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw
Source : BBC Swahili

SHARE THIS POST