MTOTO ZULKAYA APATIKANA/ALIYEMUIBA ALITAKA APEWE NYUMBA NA MILIONI HAMSINI
Agosti 8,2024 ilitolewa taarifa Polisi kuwa, huko katika Kijiji cha Jaribu Mpakani Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Kipolisi Rufiji mtoto mmoja wa kike aitwaye Zulkaiya Seif Ndambwe miaka 4 amepotea. Taarifa za kupotea mtoto huyo zilisambaa pia kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya watu walitoa maoni mblimbali, matamshi na maneno chanya na hasi. Uchunguzi wa awali ulibainisha kuwa, mtoto huyo alichukuliwa na Mwanamke mmoja mweupe alipokuwa anacheza na watoto wenzake. Jeshi la Polisi lilipokea taarifa nyingi na baada ya kuzichambua kwa kina nyingi zilibainika si za kweli, zingine zilikuwa ni za kutaka kulipiza kisasi na nyingine zilikuwa ni kutaka kusambaratisha familia. Kwa vile Jeshi la Polisi lilikuwa limesambaza taarifa za kupotea kwa mtoto huyo maeneo mbalimbali, Agosti 23,2024 zilipokelewa taarifa kutoka kwa raia wema kuwa mtoto huyo amepatikana huko Mikwambe Jijini Dar es Salaam akiwa na Mama mmoja. Askari baada ya kupokea taarifa hiyo walifanikiwa kumkamata Zakia Mohamed Timu, Miaka 26, Mdengereko, Mkazi wa Mikwambe Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es salaam akiwa na mtoto Zulkaiya Seif Ndambwe ambaye aliripotiwa kupotea toka Agosti 8,2024. Amekiri kumwiba mtoto huyo na kutokana na kukutwa naye na kwa kukiri kwake anaendelea kushikiliwa ili kukamilisha uchunguzi. Aidha, imebainika kilichomfanya kufanya tukio hilo ni baada ya kupata taarifa ya mtu aliyekuwa anatafuta mtoto asiye na wazazi na anaishi katika mazingira magum ili aweze kufuata taratibu za kumwasili. Kutokana na tamaa zake yeye akaona ni dili amepata na akisukumwa na tamaa hizo akaenda kuiba mtoto huyo. Alipoambiwa waanze kufuata taratibu na kutakiwa alete wanandug wengine, vyeti na waende kwa kiongozi wa Serikali za Mitaa kwa utambuzi alianza kusita na kushindwa kutekeleza masharti hayo, ndipo mashaka yakaanza na kupelekea kumtilia shaka. Mashaka mengine yalijitokeza pale alipoanza kudai ajengewe nyumba ya vyumba vitatu au apewe milioni hamsini. Nimezungumza na Mama wa Mtoto baada ya kukabidhiwa Mtoto wake na ameelezea kwa urefu ilivyokuwa hadi kuja kumpata mtoto wake... #geahhabibu #geahtv