Na. Catherine Sungura, Mbeya
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa ameitaka Bodi Mpya ya Ushauri ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuwasaidia na kuwashauri watendaji wafanye kazi vizuri ili kuhakikisha anayoyaota Mhe. Rais kwa Watanzania yanatimia.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakala huo ulofanyika jijijni Mbeya.
“Mwenyekiti wa bodi mutakuwa na kazi kubwa ya kuwashauri watendaji hawa, niwaombe mtusaidie na kutushauri kwani wananchi wanataka barabara na bajeti ya TARURA imeongezeka kutoka milioni 200 hadi kufika Tilioni 1.3”.
Hata hivyo ameitaka bodi hiyo kuwa wabunifu na kujipanga ili barabara zinazosimamiwa na TARURA zikamilike pia washirikiane na wataalam kuhakikisha mchakato wa kuanzishwa kwa hati fungani unakamilika na kuzinduliwa ili kuwasaidia wakandarasi wazawa.
Aidha, Waziri Mchengerwa ameipongeza TARURA kwa kazi kubwa walizofanya nchini za ujenzi na matengenezo ya barabara na madaraja licha ya kusombwa na maji wakati wa mafuriko.
“Nimpongeze Mtendaji Mkuu kwa kazi nzuri anayofanya,pongezi hizi zishuke hadi kwa watumishi wa chini kwani matokeo ya kazi nzuri zinaonekana kwa wananchi.
“Tuna kazi kubwa ya kufanya kwa Taifa letu bidii na kujitolea inahitajika, tumefanya kazi kubwa na nzuri ila yakaja mafuriko yakasomba barabara na madaraja,kwa sasa hakikisheni tunajenga upya barabara na madaraja “Aliongeza
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii Mhe. Justine Nyamoga alisema kamati yake itatoa ushirikiano ili kuleta tija kwa wananchi na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi.
Wakati huo huo Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff alisema bodi hiyo ni ya pili tangu kuanzishwa kwa Wakala huo.
Pia jukumu kubwa la Bodi ya Ushauri ni kumshauru Waziri OR-TAMISEMI kwenye mipango ya kimkakati, namna ya kufikia malengo, upangaji wa vipaumbele, mipango ya bajeti, tathimini na ufuatiliaji wa taarifa mbalimbali za utendaji kazi pamoja na maeneo mengine ya TARURA.