Mazishi ya watoto waliouwawa kwenye milima ya Golan yafanyika Jumapili

4 months ago 197

Maelfu ya waombolezaji Jumapili wamehudhuria mazishi ya watoto 12, na vijana waliouwawa na roketi kwenye eneo la Isreal linalokaliwa la milima ya Golan, wakati Israel ikiapa kujibu vikali kundi la Hezbollah la Lebanon, lililofanya shambulizi hilo.

Hata hivyo Hezbollah limekanusha kuhusika na shambulizi hilo la Majdal Shams, likiwa baya zaidi ndani ya Israel au maeneo yanayokaliwa, tangu shambulizi la Hamas la Oktoba 7 dhidi ya Israel, lililopelekea vita vya Gaza, ambavyo sasa vimeenea kwenye maeneo mengine, kukiwa na hofu ya kusambaa kikanda.

Familia na marafiki wamefanya mazishi kwenye kijiji cha Druze, kwenye milima ya Golan, sehemu ilionyakuliwa na Israel kutoka kwa Syria, wakati wa vita vya Mashariki ya Kati vya 1967, hatua ilyopingwa na kutotambuliwa na mataifa mengi ulimwenguni.

Ndege za kijeshi za Israel zimeshambulia kusini mwa Lebanon usiku kucha, huku mashambulizi zaidi yakitarajiwa kufuatia kurejea kwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kutoka ziara yake ya Marekani. Kiongozi huyo baadaye Jumapili, anatarajiwa kukutana na baraza lake la usalama.

Vikosi vya Israel katika miezi ya karibuni vimekuwa vikishambuliana na wapiganaji wa Hezbopllah kusini mwa Lebanon, lakini pande zote mbili zinaonekana kujiepusha na kile kinachoweza kuwa vita kamili, na kuhusisha mataifa mengine yenye nguvu kama Iran na Marekani.

Source : VOA Swahili

SHARE THIS POST