MAUAJI!! Amuua mke wake, naye ajiuwa kwa kunywa vidonge na konyagi, mapenzi yatajwa chanzo

1 month ago 10


Wakazi wa mtaa wa Nyamhongolo wilayani Ilemela Mkoa wa Mwanza ambao ni mke na mume wamefariki dunia nyakati tofauti baada ya kuzuka ugomvi unaodaiwa kuchochewa na wivu wa mapenzi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne Oktoba 2, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa watu hao ni Rausa Mohamed (36) aliyefariki Septemba 28, mwaka huu wakati akipatiwa matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kusukumwa na kuanguka kwenye sakafu kisha kujeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mme wake, Dervinus Nkabatina (46). Mutafungwa amesema baada ya tukio hilo majirani walifika kwa ajili ya kutoa msaada na taarifa zilifika jeshi la polisi ambapo mgonjwa alipelekwa katika kituo cha afya Igoma lakini wakati madaktari wakijaribu kuokoa maisha yake alifariki dunia. Katika hatua nyingine, Mutafungwa amesema jana Oktoba Mosi, 2024 jeshi hilo limewafikisha mahakamani watuhumiwa, Robart Kabota na wenzake watatu ambao walihusika katika ajali ya mtumbwi uliozama Septemba 25, mwaka huu wilayani Ilemela, Mwanza na kusababisha vifo vya watu tisa na wengine 29 kunusurika kifo.
Source : Mwananchi Digital

SHARE THIS POST