Mashariki ya Kati iko katika hatihati ya vita kamili ya kikanda: UN

1 month ago 14

Akihutubia wajumbe wa Baraza hilo Mkuu wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo amesema "Kutokuwa na uwezo wa pamoja kwa upande wa jumuiya ya kimataifa kukomesha mapigano yanayoendelea nchini Lebanon na kukomesha umwagaji damu, ni kitu kibaya sana. Eneo lote la Mashariki ya Kati sasa linaelekea kwenye ukingo wa vita vya hali ya juu."

Amesema wanamgambo lazima waache kuvurumisha makombora ndani ya Israel, wakati  huohuo Israel lazima iondoe vikosi vyake vya ardhini na kukomesha mashambulizi ya mabomu ya jirani zake”.

Kuchagua diplomasia badala ya silaha

Bi. DiCarlo ameongeza kuwa "Pande zote katika mzozo lazima zichukue chaguzi za kidiplomasia zilizowekwa mezani mbele yao, sio silaha zilizo kando yao."

Amesisitiza kwamba serikali huru ya Lebanon lazima iwe na udhibiti wa silaha zote katika eneo lake na viongozi lazima "wachukue hatua madhubuti za kushughulikia ombwe lililosababishwa na mkwamo wa kisiasa wa miaka mingi huko Beirut.”

Rosemary DiCarlo, Naibu Katibu Mkuu wa Masuala ya Kisiasa na ujenzi wa amani, akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Mashariki ya Kati.

Rosemary DiCarlo, Naibu Katibu Mkuu wa Masuala ya Kisiasa na ujenzi wa amani, akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Mashariki ya Kati.

Kuongezeka kwa mapigano kumezua 'dharura ya kibinadamu Lebanon

Mkuu huyo wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo amewaambia wajumbe wa Baraza kuwa mapigano yanayoendelea na yanayozidi kuongezeka kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah yamezua dharura ya kibinadamu kote Lebanon.

Hezbollah imeongeza mashambulizi dhidi ya Israel yanayolenga miji ya kusini huku Israel ikishambulia mji mkuu Beirut na mamia ya walengwa "wengi katika maeneo yenye wakazi wengi na kusababisha uharibifu mkubwa, watu kufurushwa na mateso."

Idadi ya vifo inaongezeka

Ameendelea kusema kwamba "Operesheni za ardhini za Israeli kusini mwa Lebanon zimesababisha mapigano makubwa na kuongezeka kwa idadi ya vifo kati ya Walebanon na watu zaidi ya 300 waliuawa katika wiki moja pekee.”

Robo ya nchi sasa iko chini ya kile kinachoitwa amri za kuhama zilizotolewa na vikosi vya Israeli na wengine kupewa notisi ya chini ya saa mbili kuondoka, mara nyingi katikati ya usiku amesema Bi DiCarlo.

Amezitaka Nchi Wanachama kuchangia ombi la Umoja wa Mataifa la dola milioni  425 lililozinduliwa wiki iliyopita "Nawashukuru wale ambao tayari mmetoa au kuahidi msaada."

Mbali na wajumbe 15 wa Baraza ambao watachukua nafasi hiyo ya kuzungumza kufuatia mkutano huo, wawakilishi kutoka Lebanon, Indonesia, Israel, Mauritania, Syria na Iran pia wanatarajiwa kutoa taarifa pamoja na mwakilishi kutoka Muunganowa wa Ulaya.

Tishio kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa

Jean-Pierre Lacroix  ambaye ni mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mattaifa akizungumzambele ya wajumbe hao wa Baraza la Usalama amesema kadiri mzozo unavyozidi, ikiwa ni pamoja na mizinga na silaha ndogo ndogo, mashambulizi ya anga, uvamizi wa ndege zisizo na rubani na milipuko mingi walinda amani wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL, wamewekwa  katika hatari kubwa.

Amesisitiza kwamba mapema leo walinda amani wawili walijeruhiwa wakati kituo cha uchunguzi katika makao makuu ya UNIFIL huko Naqoura, kusini mwa Lebanon, kilipopigwa na kombora.

Ameongeza kuwa Jeshi la Ulinzi la Israel limeweka kituo karibu mkabala na kituo cha  Umoja wa Mataifa Umoja "hatua ambayo tunapinga vikali."

Baadhi ya walinda amani, amesema, walikuwa wamehamishwa kwa muda kwani ulinzi na usalama wao unazidi kuwa hatarini.

Bwana. Lacroix ametoa wito kwa mamlaka ya Israel "kuheshimu hadhi ya ulinzi ya UNIFIL na wafanyakazi wake, ikiwa ni pamoja na kutokiuka ulinzi kwa majengo ya Umoja wa Mataifa."

Jean-Pierre Lacroix, Naibu Katibu Mkuu wa Operesheni za Amani, akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Mashariki ya Kati.

Jean-Pierre Lacroix, Naibu Katibu Mkuu wa Operesheni za Amani, akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Mashariki ya Kati.

Maeneo ya operesheni za UN hayana watu na yanazidi kutokalika

Jean-Pierre Lacroix ambaye ni wa pili kati ya maafisa wawili wakuu wa Umoja wa Mataifa kuhutubia mkutano huo w Baraza la Usalama leo ameliambia Baraza hilo kwamba sehemu kubwa ya kusini mwa Lebanon ambako ujumbe wa kulinda amani wa UNIFIL unafanya kazi "sasa halina watu na linazidi kutokalika".

Ameongeza kuwa wakati operesheni za ardhini za Jeshi la Israel nchini Lebanon zikiendelea, Hezbollah nayo inaanzisha mashambulizi katika eneo la msitari wa Bluu "na kutishia vituo vikubwa vya watu nchini Israel kwa silaha za hali ya juu".

Bwana Lacroix ameongeza kuwa tangu mwanzoni mwa mwezi "kumekuwa na mapigano makali ardhini, huku takriban wanajeshi 12 wa Israel na wapiganaji wengi wa Hezbollah wakiripotiwa kuuawa.

Source : UN Habari

SHARE THIS POST