Liverpool yaanza mazungumzo na Salah

2 months ago 219

Klabu ya Liverpool imeanza mazungumzo wawakilishi wa mshambuliaji wao raia wa Misri, Mohamed Salah, 32, kwa ajili ya kumsainisha mkataba mpya lakini hadi sasa hakuna dalili ya kufikia mwafaka.

Salah amekuwa akihusishwa na timu mbalimbali za Saudi Arabia ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili tangu dirisha kubwa la mwaka jana.

Al Ittihad ilikuwa  ni moja kati ya timu zilizohitaji kumsajili Salah na iliweka mezani ofa ya mshahara unaofikia Pauni 70 milioni kwa mwaka lakini ilishindikana.

Licha ya mazungumzo hayo yaliyoanza hivi karibuni uwezekano wa Salah kubakia unaonekana kuwa mdogo kwani kiasi cha mshahara anachohitaji ili asaini mkataba mpya ni kikubwa.

Benchi la ufundi la Liverpool halihitaji kuona Salah akiondoka na msimu huu amecheza mechi 17 za michuano yote na kufunga mabao 10 na kutoa asisti 10.

Source : Millardayo.com

SHARE THIS POST