Lawi atishiwa kupelekwa mahakamani kisa malipo ya usajili

3 months ago 37


Wakati sakata la usajili wake kwenda Simba likiwa halijapata mwafaka, beki Lameck Lawi ameibua msala mwingine baada ya aliyekuwa mlezi wake, Mlinda Lusana kudai kuambulia patupu kwenye mauzo yake. Mlinda amesema mchezaji huyo hapokei simu, huku akitishia kumburuza mahakamani. Mlinda ambaye ni mkurugenzi wa Kituo cha Kukuza Vipaji vya Soka cha Misungwi, mkoani Mwanza amesema aliingia makubaliano ya kunufaika na asilimia 10 ya mauzo ya mchezaji huyo, lakini mpaka sasa hajaambuliwa chochote tangu aliponunuliwa na Coastal Union kutoka Copco FC hadi sasa ambapo anadaiwa yupo Ubeligiji alikoenda kucheza soka la kulipwa. Juhudi za kumtafuta Lawi ili kuzungumzia madai hayo bado zinaendelea. Endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi.
Source : Mwananchi Digital

SHARE THIS POST