Kwanini hauhitaji tena 'kava" la simu yako?

Chanzo cha picha, Getty Images
Simu za mkononi za kisasa aina ya smartphone ama simu za rununu, zimeboreshwa kimuundo na kiteknolojia huku zinazotengenezwa hivi maajuzi, zina wekwa 'makava' kwa kiswahili sanifu vifuniko vigumu kuzuia kuharibika zinapoangushwa chini.
Hali ambayo imewafanya wengi kuuliza swali kama makava ama vifuniko tunavyotegemea kulinda simu na kuzuia hasara zinapoanguka, kama vina umuhimu mkubwa.
Mwandishi wa BBC alishiriki katika mpango wa baadhi ya watumizi wanaosusia kutumia makava ama vifuniko kudhibiti hasara dhidi ya simu zao za mkononi. Katika zoezi hilo, alishirikiakana na wataalamu na kuangazia ikiwa upande uliotengezwa kwa glasi ungeharibika vibaya katika jaribio hilo.
Miezi michache iliyopita, nilifika katika duka la kuuza bidhaa za kielektroniki zinazotengenezwa na kampuni ya Marekani ya Apple, kwa ajili ya kununuwa aina mpya ya simu ya Iphone.
Baada ya kutathmini kwa kina na kuangalia aina za simu ambazo zilikuwa dukani, mhudumu wa mauozo dukani humo alinialeza kwamba bei ya simu niliyoichagua ilikuwa dola 1,199 za Kimarekani ambazo ningelazimika kulipa kwa ajili ya kupokezwa simu hiyo. Alicheka nilipomuambia kwamba gharama hiyo ni sawia na kodi ya nyumba ninayolipa kila mwezi. " Ajabu, sio!" alisema. "Wacha sasa tuangazie mifuko au vifuniko vya simu yako."
Ilikuwa jambo la wazi kwamba hatua ya kufuatia ni ya kununua mfuko . Ila huku bei ya simu za rununu ikipanda maradufu na kuzidi kuwastaajabisha watumizi kote ulimwenguni, baadhi ya wateja wanafuata mkondo tofauti: wanatumia simu zao bila ya kuhitaji mifuko au vifuniko vya usalama
Hali ambayo wakati mmoja ingehisiwa kuhataraisha usalama was imu hizo hasa, wanapotembea na kufanya kazi katika maeneo yenye sakafu ya saruji, au kumwagikiwa maji au vinywaji na vile vile kupata vumbi. Kunao baadhi ambao hata hawatumii vifaa maalum vya kuzuia sura ya simu kuharibika yaani {screen protectors}. Ninawafahamu baadhi ya watu wenye kuchukuwa hatua hii. Simu zao zimeng'aa, na ziko na fremu za titanium ambayo ni aina maalum ya gilasi ambayo inawezesha simu yako kuonekana vyema pande zote. Wanaonekana wenye Kujawa na furaha kubwa na wenye kutojali kuhusu hasara. Je, hili limejikita akilini mwangu pekee ama ndio hali halisi? Kwamba kuna simu ambazo hazihitaji mifuko ya kuzuia hasara ya kuharibiwa?Nina hisi kwamba ni hofu inayosimama kati yangu na mimi kuweza kuishi maisha yasiyojawa na wasiwasi.
"Hebu jishuhudie mwenyewe, ishike simu na uhisi mwenyewe jinsi ilivyo, Rafiki yangu alinieleza wiki chache baada ya tukio la pale dukani. Ni mwenye kujivunia hali ya kwamba simu yake haina mfuko, na alinionyesha simu yake ya aina ya Iphone. Ilionekana yenye urembo zaidi ilivyokuwa bila ya kufunikwa au kuwa kwenye mfuko, n ahata ilihisi vyema zaidi nilipoibeba mkononi mwangu. Simu zinazotengezwa sasa, ni zenye upande wan je mgumu . Nimeiangusha simu yangu mara kadhaa, bila ya kuvunjika au kuharibika, na ipo sawa tu."

Chanzo cha picha, Isa Zapata
Kwa mujibu wa mazungunmzo niliyoyafanya na watengenezaji vioo vya simu , watu wanaolipwa kuharibu simu na amba oni wapnezi wa matumizi ya simu bila mifuko , huenda anachokisema ni sawa.
Wataalamu wanakubaliana na wazo hilo kwamba simu za kisasa za mkononi zimeboreshwa zaidi kuliko za hapo awali. Hata hivyo, wengi ambao ninawafahamu bado huweka mifuko kwenye zimu zao kwa ajili ya kuzilinda dhidi ya hasara. Kwa hilo, Ni nani aliye saw ana ni nani mwenye wazimu?
Nimaamuwa kufanya tathmini ya kina. Nilipofika nyumbvani, nilivua mfuko was imu yangu, nikauweka kwenye kabati na kuamua kutumia simu yangu bila ya mfuko kwa muda wa mwezi mmoja katika hali hii ya maisha bila wasiwasi wa kuhofia simu kuharibika.
Nilipomuandikia mhariri wangu pendekezo la kufanya utafiti huu kwa ajili ya kuaandaa taarifa, alipendezwa na wazo hilo ila alinihakikshia kwamba BBC haingenilipia gharama ya kuitengeneza simu ikiwa ingeharibika . Naiombea nafsi yangu, Mola ainusuru majanga.
Kioo kuvunjika
Kumekuwa na mazungumzo makubwa kuhusu namna ambavyo hali hii ya kutotumia mifuniko ya kufunika simu imekuwa kama hadhi katika jamii kwa wengi wanaohisi kwamba wanataka kutambulika kama wenye staha na ukakamavu. Ninapowahoji wataalamau wa masualaya teknolojia, kwa pamoja na wakurugenzi na wajasiriamali katika sekta hiyo, ni nadra sana kuwaona na simu zilizovalishwa mifuko ya kuzuia hasara.
"Unasema kwamba , ninaweza kugharamia shughuli nzima ya kuifanyia simu hii marekebisho ikiwa itaharibika. Ila sio kwa sababu ya mtazamo tu. Nilikuwa mmoja wa wanaokosa kutumia mifuko kwenye simu hata kabla ya kuanzisha biashara yangu," alisema Yousef Ali, ambaye ni afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Blast Radio, ambayo inapeperusha matangazo ya redio mitandaoni hususan kuwafaa ma DJ wa muziki wanaotaka kuonyesha utaalamu wao kwa wasikilizaji. Ni kama kuweka kifuniko cha aina ya VYNIL kwenye viti vyako vya nyumbani kwa ajili ya kuvilinda dhidi ya kuharibiwa.
Ninazo suruali zilizonunuliwa kwa bei ghali, hilo linamaanisha kwamba kuna haja ya mimi kuvalia suruali nyengine juu ya hiyo kwa ajili ya kuilinda dhidi ya kuharibika? Haya yana mwisho kweli?
Sitakuficha kwani katika wiki ya kwanza, ambapo sikuwa na mfuko wa kulinda siku yangu, nilijwa na wasi wasi na sikujihisi vyema kabisa. Ni njia mbaya kabisa ya kutishia ajali kutokea au hasara kupatikana. Ila mitindo haikai kwa muda mrefu. Ninachokihitaji ni Ushahidi wa kikamilifu - kimsingi, eneo ngumu zaidi ambapo ninaona simu yangu ikiangukia, ambayo ni hatari kuliko sakafu ya saruji.
"Ni kweli kwamba hauna haja ya kuivalisha simu yako mfuko wa kuilinda. Ila, suala la wazi ni je, wewe ni mcheza kamari? anasema Rich Fisco.
Ikiwa unaisoma taarifa hiyo kwa simu yako ya mkononi, huenda unaitazamia kupitia GORILLA GLASS ambayo ni kifaa maalum kilicho pakwaa rangi ngumu inayong'aa sana, na ambayo imetengenezwa na teknolojia ya kisasa inayozuia simu kuharibika vibaya na kampuni ya Corning.
Makampuni makubwa duniani ya kutengeneza simu za mkononiyanatumia Gorilla glass au bihdaa nyingine inayotengenzwa na kampuni ya Carning – kwa baadhi au simu zote – hasa kutengeneza skrini.
Makampuni kama vile Apple, Google , Huawei na Samsung yote yanategemea utalaamu huu. Kuna baadhi ya simu ambazo hazijatumia teknolojia hii, hasa zilizotengenezwa mapema kidogo na vile vile aina za simu ambazo zinatengenezwa kwa gharama ya chini. Ila kwa jumla, Corning imetegemewa kutengeneza simu za kisasa.
Mpangilio wa kutengeza Gorilla glass huanza kwa kuweka glasi katika chumvi ilioyeyushwa baada ya kuwekewa kwenye moto uliofikia joto la digrii 400C. " Chumvi iliyeyushwa huvuta vipande vidogo wa chuma aina ya Lithium kutoka kwa glasi na kuweka viwango vikubwa vya madini aina ya Potassium," alisema Lori Hamilton, mkurugenzi wa taknolojia ya Gorilla Glass katika kampuni ya Corning. "
Inaunda safu iliyongumu ambayo inafanya simu kuwa thabiti na kuzuia mapungufu kuwepo kwenye glasi hiyo ya simu," Yaani tun maamnisha kwamba , inaifinya glasi hiyo pamoja, na kuifanya kuwa thabiti na kustahmili athari ya kuanguka.
Utafiti wa kampuni ya Corning inajumuisha kuziharibu simu kwa kutumia mbinu mbali mbali kwa ajili ya kupata kuelewa jinsi zinavyoharibika na hali ya kuzia hilo.
Simu huwekwa kwenye mashine maalum zinazokwarusa glasi ya skrini zao, na vile vile kuwekwa kwenye mabomba kwa pamoja na vifunguu vya gari kwa ajili ya kuigiza hali ya kuwa kwenye mifuko. Corning pia hukusanya simu ambazo zimeharibiwa na wateja na watumiaji kwa ajili ya kufanya tathmini zaidi kuhusu zilizvyoharibiwa.

Chanzo cha picha, Isa Zapata
"Kisha huwa tunaangazia kwa kina utafiti huo wa aina ya CSI ambao unafahamika kama utafiti wa mvunjiko {fracture analysis} ambapo tunaangalia vipande vidogo vya glasi kuelewa chanzo halisi cha kuvunjika kwa simu," alisema Hamilton.
Wakati ambapo simu yako inavunjika, Ni skrini ambayo huharibika wakati mwingi. Ila, kulingana na Hamilton, matokeo yameonyessha kwamba hali imaimarika kwa kiwango kikubwa katika miaka ya hivi maajuzi, simu za mkononi za kisasa almaarufu smartphones ni zenye nguvu.
Mnamo 2016, Corning ilitoa ripoti ya kuonyesha kwamba simu zilizotengenezwa kwa aina ya glasi ya Gorilla glass 5 zilistahmili athari zilipoangushwa umbali wa mita moja katika maabara. Kiwango hicho kilipanda hadi uwezo was imu hizo kustahmili makali ya kuanguka kwa kina cha mita 2 kwa kutumia teknolojia ya kutengeneza glasi ya Gorilla Glass Victus. Gorilla Armor 2 ambayo ni mojawapo ya teknolojia mpya inayotengenezwa na Corning ambayo imetumika kutengeneza simu yam konini ya Samsung Ultra S25 na ambayo ina weza kustahmili makali ya kuangushwa kwa umbali wa mita 2.2 chini.
Ushahidi wa nje unaonyesha kwamba unaunga mkono wazo wkamba maboresho katika viungo asili vya kunegeneza simu za mkononi za kisasa yameathiri vyema muundo na muonekano was imu hizo.
Mnamo 2024, kampuni ya bima ya All State, ambayo inauza bima ya kuwakinga watumiaji dhidi ya hasara, wanapopatwa na ajali , ilipata kwamba Wamakenai milioni 78 waliripoti visa vya simu zao kuharibika ikilinganishwa na milioni 87 mwaka wa 2020.
"Hatutumii neno kwamba haiwezi kuvunjika," alisema Hamilton. " Mapungufu hayakosekani.
Kutakuwa na uwezekano wa kupatikana kwa upungufu unaoathiri uwezo wa simu kufanya kazi ." Ila Hamilton anasema kutotumia mfuko, si jambo baya sana kwa wakati huu, kama ni jambo ambalo mwenye kutumia simu amelipendelea. "Mwisho wa kwisha, ni kwamba simu ni hatua ya uwekezaji ," alisema. " Sina chochote kinachozuia hasara kwa skrini ya simu yangu yaani Screen Protector, lakini ninatumia mfuko." "Japo sio mfuko wa kutumika kama ulinzi was imu yangu, ni wa aina ya wallet – wa kuhifadhi vitu vingine pia, kama vile kadi za benki na pesa."
Imenifanya kuwa makini kuhusu jambo moja
Gorilla glass, ilibuniwa kwa ajili ya matumizi kwenye simu ya Iphone, na kupitia teknolojia zake mpya, aina mpya za simu hiyo zinatumia mfumo huo ulioboreshwa, ambao unatambulika kama ceramic shield ambao unatengenezwa na kampuni ya Corning. Apple imedai kwamba aina hii mpya ya teknolojia hii ya Ceramic Shield iliyotumika kutengeneza Iphone 16 inaifanya kuwa na nguvu zaidi ya mara mbili na kwamba glasi yake haiwezi kufananhishwa nay a simu nyingine ya mkononi.
QUOTE: Nina suruali za bei ya juu, hii ina maana kwamba ni lazima nivalie suruali nyingine juu kwa ajili ya kuzuia hasara kwa zenye ghara ya juu? Mwisho wake ni upi? – Yousef Ali
Kampuni ya Apple itasifia mazuri ya teknolojia hii ya ceramics, na wakati huo huo pia, itakuuzia mfuko wa kusitiri simu yako wenye nembo ya kampuni hiyo.
Aliyeniuzia simu yangu ya Iphone, alipendekeza kwamba ninunwe mfuko wa rangi ya samawati kwa bei ya dola 49 za kimarekani. Kwa hivyo, kuna muhimu kwa mtu kuwa na mfuko wa kuhifadhi simu yako? Apple ilikataa kujibu suali hilo.
Kampuni ya kutengeneza mifuko ya simu ya Spiegen, kwa upande mwingine ilikuwa tayari kuzungumza. "Ni kweli kwamba simu za mkononi za kisasa zimeboreshwa zaidi," alisema Justin Ma, msemaji wa Spigen."hata hivyo, japo kuna mabadiliko ya aina hii kiteknolojia, bidhaa hizi hazi hazina uhakika wa kutoharibika kabisa," alisema.
Na hata ma anasema kwamba suala la mifuko ya simus io la lazima. "Utatarajia mtu kusema kwamba kila mwenye kumiliki simu anahitaji mfuko wa kulinda usalama wake, ila hali halisi ni kwamba hili litetegemea mtu binafsi.
"Baadhi watapendelea hilo, na wengine wanavutiwa na simu yao kuwa kama ilivyotengenezwa na kuna wengine ambao wangependa kuzuia hasara kubwa kwa kuhifadhi vyema simu zao. Wengine hufanya hivyo kwa ajili ya mapambo tu.
Maamuzi haya yakiwa tofauti kabisa, wanaopenda mifuko kwa ajili ya kuhifadhi simu wananafasi nzuri ya kukaa na simu kwa muda. Ma anasema kwamba kampuni ya Spigen hutengeneza mifuko ambayo inatumiwa kuhifadhi simu za mkononi zaidi ya milioni mia moja. Kampuni nyingine ya Towards Packaging ilifanya mauzo ya dola milioni 25 za kimarekani ya mifuko ya siku ya Ihone pekee mwaka wa 2024.
Nilikuwa jikoni mwangu nikinywa maji kwenye bilauri ya glasi, nilipopatwa na wazo la kutazama simu yangu kwa muda kabla ya kupata usingizi. Nilipoiondoa simu yangu mfukoni, vidole vyangu vilishindwa kuidhibiti . simu hiyo iliruka hewani, na kugonga upande wa jokofu langu na kuanguka chini kwa nguvu, karibu na miguu yangu.
Nilipoichukuwa na kuangalia kama ilikuwa na tatito, simu ilikuwa sawa, hali ninayohisi ilisaidiwa na glasi ngumu , au huenda ni bahati ama kwamba sakafu ya nyumbani kwangu sio ngumu.
QUOTE: Kutotumia mifuko kumenifanya kuwa makini kuhusu jambo moja, ambapo ninajipata sina wasiwasi mkubwa kuhusu usalama was imu kama ilivykuwa awali. Siamini kwamba ni mimi niazungumza hivi, ila ninaitumia simu yangu kwa kiwango cha chini sasa – Jonna Valenti
Kwa Jonan Valenti, mmoja wa wanandoa wanaoishi katika jimbo la Noth Carolina nchini Marekani, kutumia simu bila ya mfuko ilikuwa uamuzi uliotokana na mengine na wala sio sayansi au hadhi katika jamii. " Nilipoinunuwa simu yangu , binti yangu alichagua yenye rangi ya waridi. Na sikutaka kuvalisha mfuko kwa sababu ilinipendeza sana," alisema.
Valenti hakurejea katika hali yake ya awali, tangu hapo si mwenye kutumia mifuko ya kihifadhi simu, nah atua hiyo ilibadili uhusiano wake na simu yake. " Kwa sababu vidole vyangu havina uthabiti, niko makini kabisa," alisema. "Imenifanya kuwa makini kuhusu jambo moja, kwamba sifuati mkondo wa wengi bila ya kuwazia kwa kina. Siamini kwamba ni mimi ninazungumza hivi, ila ninatumia simu yangu kwa kiwango cha chini sasa."
Japo Valenti anazungumza mambo yenye kuwavutia wengi, siwezi kumuunga mkono. Kwa upande wangu, sijapunguza matumizi ya mtandao wa internet kwa simu yangu.
Kuanguka
Nilipoanza kazi ya uandishi, nilifanya kazi katika jarida la Magazine Cosnumer Reports, ambapo kulikuwa na maabara kamlili penye wahandisi wamebuni na kutengeneza na kutathmini ubora wa bidhaa kwa zaidi ya miongo tisa. Katika ofisi ambayo haikuwa mbali na ofisi yangu nilipokaa, kundi la wahandisi lilifanyia uchunguzi aina mbali mbali za simu za mkononi kwa miaka mingi. Walichunguza ubora kwa kutumia mbinu kali. Na ikiwa kuna mwenye kufahamu ukweli ni mfanyakazi mwenzangu wa zamani Rich Fisco.
"Tunaitambulika kama tathmini ya kuangusha – yaani The drop test," alisma Fisco ambaye anasimamia kitengo cha tathmini ya bidhaa za Kielktroniki . Simu huwekwa kwenye kasha la chuma lenye urefu wa futi 3 ambalo lina vipande vya saruji katika pande zote, alisema.
Kisha kasha hilo huzungushwa zaidi ya mara 50, na kugongesha simu dhidi ya saruji ten ana tena. Shughuli inapokamilika, mhandishi hutazama kujuwa jinsi simu ilivyo. Ikiwa itaatshmili makali ya shughuli hiyo, Fisco anasema kwamba wanarejesha simu hiyo kwenye kasha kwa mara ya pili kwa mizunguko mengine 50.
PICHA: kutotumia mifuko ya simu imekuwa jambo la utambulisho wa hadhi katika jamii katika baadhi ya maeneo. (Credit – Isa Zapata)
"Wakati ambapo tathmini ya kuangusha ilipoanzishwa , thuluthi moja ya jumla ya simu zilizopitia mchujo huu, zilishindwa kupita mtihani huu." Alisema Fisco. " Hatujaona simu iliyokosa kupita tathmini hii ya kuangusha kwa muda mrefu sana. Glasi inayotumika ni ya kiwango cha juu. Siku hizi wanaotengeneza simu wanaonekana kufanya kazi nzuri kabisa.
"SImaanishi kwamba simu haitokosa kukwaruzika Skrini katika maisha ya kutumika na ikiwa utaiangusha simu na iangukie jiwe pabaya, basi unaweza kuipungia mkono. Ikiwa simu yako itaanguka barabarani , huenda ikavunjika," Fisco alisema. " Ni ukweli, sio lazima utumie mfuko wa kuhifadhi simu, ila suali ni kuwamba je wewe ni mcheza kamari?"
Na japo Fisco huandaa ripoti za kuonyesha ubora was imu anazozifanyia utafiti wa tathmini ya kuangusha kila mwaka, anasema kwamba simy yake ya kibinasfi inatumia mfuko wa kuhifadhi. " Bila shaka ninatumia, Mimi sipendi kugharamika."
Nilikuwa ninaondoka nyumbani katika simu ya 26 ya mwezi ambao nilipangia kutumia simu bila ya kuwekwa mfuko wa kuhifadhi. Nilipokuwa katika ngazi ya juu ya jengo ninaloishi, nilishika simu yangu kufuatilia shughuli za usafiri wa kuelekea kazini. Sielewi kilichotendeka kwani huande nilikuwa mwenye kutokuwa na umakini – kwa sababu ghafla, simu yangu ilikuwa haipo mkononi wmangu, na ilikuwa inaanguka kwenye ngazi mara kadhaa kabla ya kusimama kule chini ya ngazi hizo.
Nilikimbia mbio kuiangalia kama ilikuwa na jambo, cha ajabu ni kwamba ilikuwa imekwaruzika kidogo tu upande mmoja na wala haikuw ana tatizo kubwa.
Nilimaliza utafiti wangu katika siku zilizofuatia nikiwa mwenye makini sana, kila mara nikiishikilia simu yangu kwa nguvu popote nilipokuwa na kuwa makini nilipoichukuwa kutoka chini au kuiweka popote.
Rafiki yangu hakubahatika kama mimi, nilipokutana naye mjini, nilimjulia alikuwa anaendelea vipi na akanijibu kwamba alikuwa anahisi vibaya.
"simu yangu ilianguka, ikavunjika, na kupasuka vipande kwenye kamera yake" Alikuwa wa kwanza kuitaja jambo hilo kama kinaya. Hata hiyo simu yake ni ya kitambo kidogo kwa hivyo teknolojia yake sio kama hii yangu. Huenda aina mpya ya ceramic glass huenda ikaokoa simu yake , pale ilipoanguka. Au la
Na japo utafikiria kuzamisha simu yako kwenye chumvi iliyoyeyushwa , hali halisi ni kwamba glasi huvunjiika. Ila nimeamini na kushawishika kwamba aina hii mpya ya simu na uangalifu wa wenye kuzumia, kutumia mfuko ni jambo ambalo unaliamulia kibinafsi.
Kufikia mwisho wa tathmini yangu ya utafiti, nilikuwa mtulivu maana wasiwasi niliouhisi ulishuka. Nilikuwa nimeshuhudia mengi na kuwa na hali ya kushtuka mara kadhaa, huku kila mara tatizo lilipotokea, nilihisi kwamba ninapokea onyo.
Mwishioni, nimerejea matumizi ya kutumia mifuko ya kuhidfahi simu yangu. Ila mara wkamba hujipata simu imeanguka .