KUMEKUCHA! WANAWAKE WAIOMBA SERIKALI IKOMESHE BIASHARA YA UKAHABA BABATI
Wanawake wilayani Babati, mkoani Manyara, wameiomba Serikali itokomeshe biashara haramu ya ukahaba katika baadhi ya maeneo ya Mji wa Babati ambapo wamedai biashara hiyo imekuwa ikisababisha baadhi ya wanaume kutelekeza familia zao na ongezeko la matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo vipigo kwa wenza.