‘Kiongozi usifikiri nafasi yako haiwezi kuzibwa’- Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango

2 months ago 15

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewataka Viongozi wakipewa nafasi wasifikiri kuwa nafasi zao haziwezi kuzibwa ambapo amesema Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Suluhu wakati wowote anaweza kutengeneza Timu yake ya ushindi.

Akiongea mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu leo July 26,2024, Dkt. Mpango amesema “Niwapongeze wote walioteuliwa mmepewa dhamana kubwa ni matumaini ya Mh. Rais na Watanzania kwamba mtakwenda kucheza vizuri katika nafasi hizo niwaombe moja tu asije akafikiria yoyote yule nikiwemo Mimi Makamo wako Mheshimiwa Rais kwamba nafasi yangu haiwezi kuzibwa”

“Ni muhimu sana kuzingatia kama Viongozi kwamba Amiri Jeshi Mkuu wakati wowote anaweza kutengeneza Timu yake ili kupata ushindi, kuwaletea ushindi Watanzania”

Source : Millardayo.com

SHARE THIS POST