KAMPUNI YA USAFIRISHAJI SIMBA YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUTOA MAHITAJI KITUO CHA WATOTO YATIMA

1 month ago 11

KATIKA Kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja Kampuni ya Wakala wa Forodha (SIMBA) Wameikumbusha Jamii Kuhakikisha wanatoa faraja kwa watu wenye uhitaji hasa vituo vya watoto Yatima.

Akizungumza Afisa Mtendaji Mkuu wa Uendeshaji Gladness Mosha katika Kituo cha Watoto Yatima Cha Orphanage kilichopo Zinga Bagamoyo amesema Kwa Kutambua mchango mkubwa unaofanywa na wateja wao kwa Kuhakikisha wanapatiwa huduma nzuri za Usafirishaji wameona Katika Kuadhimisha Wiki hiyo wagawane kidogo na Watoto hao.

Aidha amesema mbali na Kufurahika nao Wamekabidhi Mahitaji mbalimbali ikiwemo Vyakula ,Mafuta ya Kujipaka ,Vifaa vya Shule .

Pia ameeleza namna Kampuni yao inavyotoa huduma licha ya kuwepo ushindani wa Kampuni mengi yanayotoa huduma za Usafirishaji nchini.

"Mzigo unapokuwa njiani Mteja anapewa nafasi kupata ujumbe wa kujua mzigo upo wapi na hali ya kiusalama zaidi."

Pia amewaomba Wateja wao Kuendelea kutumia Kampuni ya Simba Kuhakikisha Mizigo yao inasafirishwa kwa usalama ili kiasi kinachoingia katika Kampuni kiweze kutumika katika kusaidia Makundi yenye uhitaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo hicho cha Amani Orphane center Margareth Mwegalawa amewashukuru sana Kampuni hiyo ya Forodha kwa kuona nafasi ya kusaidia Watoto hao katika kituo hicho.

Hata hivyo ametoa wito Kwa Makampuni, Taasisi na Watu Wenye uwezo Kuwakumbuka Watoto wenye Uhitaji ili waweze kutimiza ndoto na Malengo yao.
 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Wakala wa Forodha  Gladness Mosha akikabidhi Mahitaji kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto cha Amani Orphanage center Bi.Margareth Mwegalawa Kama Sehemu ya Kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ambapo safari hii Kampuni hiyo iliamua Kutoa faraja Kwa watoto hao Bagamoyo
 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Wakala wa Forodha Gladness Mosha akizungumza na watoto mara baada ya Kugawa Mahitaji mbalimbali katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Amani center Kilichopo Bagamoyo wakati wakiadhimisha Wiki ya Huduma Kwa Wateja
 

Pichani Mahitaji Mbalimbali  yaliyotolewa na Kampuni ya Forodha Simba Clearing  kwa ajili ya Watoto wenye Uhitaji katika Kituo cha Amani Orphanage center Kilichopo Zinga Bagamoyo
 

Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto wenye Uhitaji Amani Orphanage center Margareth Mwegalawa akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea msaada kutoka Kampuni ya Wakala wa Forodha "Simba Clearing" ambao waliamua Kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kituoni hapo

Source : Michuzi Blog

SHARE THIS POST