Iran yanyonga mfungwa wa saba kwa makosa ya mauaji

3 months ago 53

Vyanzo vya haki za binadamu vinasema serekali ya Iran imemnyonga Kamran Sheikheh, mfungwa wa Kikurdi na Kisunni na mshtakiwa wa mwisho kati ya saba aliyehukumiwa kifo kwa mauaji ya 2008 ya mhubiri wa Kiislamu.

Taarifa zinasema Sheikheh alinyongwa mapema Alhamisi katika gereza la Urmia kaskazini magharibi mwa Iran.

Katika miezi ya karibuni, washtakiwa wengine sita Qasem Abesteh, Ayoub Karimi, Farhad Salimi, Davood Abdollahi, Anvar Khezri, na Khosrow Besharat, wote walinyongwa kwa kuhusika kwao katika kifo cha Abdulrahim Tina, imamu wa Msikiti wa Ukhalifa wa Rashideen mjini Mahabad.

Ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International ilisema kwamba walihukumiwa kifo “katika kesi zisizo za haki kabisa” zilizogubikwa na shutuma za kuteswa kwao ili wakiri makossa.

Kwa mujibu wa Radio Free Europe/Radio Liberty, wote saba walikanusha mashtaka dhidi yao katika barua ya wazi.

Source : VOA Swahili

SHARE THIS POST