"Iliniumiza kwasababu alikuwa ni mtu ambaye unaishi naye"
Leo imetimia mwaka mmoja tangu wanamgambo wa Hamas waliposhambulia Israel katika eneo la karibu na mpaka wa Gaza na kuua watu 1,200 na wengine 251 kuchukuliwa mateka. Miongoni mwa waliopotea na baadaye kuripotiwa kufariki baada ya shambulio hilo walikuwa wanafunzi wawili wa kilimo kutoka Tanzania ambao ni Clemence Mtenga na Joshua Mollel. Rafiki yao wa karibu, Ezekiel Kitiku, alinusurika kwenye shambulio hilo na alifanya mahojiano na mwandishi wa BBC, @lasteck2024 Alfred Lasteck alikutana naye hivi karibuni baada ya kurejea nyumbani nchini Tanzania. #bbcswahili #israel #gaza Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw