MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, leo ameongoza Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Kariakoo na kutumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa. Usafi huo uliandaliwa na TAHLISO pia ulilenga kuunga mkono agenda ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,ambaye ni kinara wa kuhifadhi mazingira. Katika kufanya usafi huo, DC Mpogolo naTAHLISO walipita katika vijiwe na kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii kutoa elimu ya umuhimu wa kujiandikisha katika Daftari la Mkazi na kupigaji kura. Mpogolo, amesema uchaguzi wa awamu hii hauhitaji mwananchi kupiga kura kwa kutumia kitambulisho cha mpigakura, bali muhimu ni kujiandikisha katikaDaftari la Mkazi. “Kila mwenye umri kuanzia miaka 18, ajitokeze kujiandikisha.Tusisubiri siku ya mwisho. Uandikishaji huu umeanza jana na utamaliziki Oktoba 20,”amesema Mpogolo. Mpogolo, amepongeza TAHLISO kwa kufanya usafi, kutoa elimu ya uchaguzi na kueleza hiyo ni ishara njema kwa taifa na kumuunga mkono Rais Dk. Samia. Rais wa TAHLISO Zainabu Kitima, amesema azma kubwa ni kuhamasisha vijanaa na watanzania kumuunga mkono Rais Dk. Samia, kuandaa mazingira. “Ili kupata kiongozi bora ni lazima kujiandikiha na kupiga kura. Tunawaomba watanzania kutuunga mkono na kuunga mkono serikali yao kuchagua viongozi wanao wataka. Zoezi hilo lilishirikisha pia wananchi, makampuni ya usafi, Jumuiya ya Wamachinga Kariakoo (KAWASO) vyombo vya ulinzi na usalama na mabalozi mbalimbali wa usafi.