China imesema Jumamosi itatoa bondi maalum kusaidia kuchochea uchumi wake unaoyumba, ikiashiria matumizi ya fedha yataimarisha mabenki, yataongeza soko la nyumba na kupunguza deni la serikali za mitaa kama sehemu ya moja ya mipango yake mikubwa sana ya afueni katika miaka kadhaa.
Mpango huo ni sehemu ya mfululizo wa hatua zinazochukuliwa na Beijing kuweka mipango katika utaratibu wa kuisaidia sekta ya biashara ya majumba ambayo kwa miaka mingi ilikuwa na matatizo, na matumizi ya chini ya muda mrefu ambayo yameikumba nchi hiyo yenye uchumi wa pili mkubwa duniani.
Bondi hizo maalum zilizopangwa na Beijing zinalenga kuboresha mtaji uliopo katika mabenki, kama sehemu ya msukumo wa kukopesha katika matumaini ya kuleta hamasa katika matumizi ya wateja ambayo si mazuri.
China pia inajiandaa kuziruhusu serikali za mitaa kukopa zaidi ili kufadhili ununuzi wa ardhi ambayo haijatumika kwa ajili ya maendeleo, kwa lengo la kuliondoa soko la nyumba ambalo limedorora kwa muda mrefu.