Blinken aomba mataifa ya ASEAN kukabiliana na changamoto za dunia

6 months ago 132

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken muda mfupi kabla ya kukutana na mwenzake wa China, Jumamosi, ameomba mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia yajikite katika kukabiliana na changamoto zilizopo, ikiwemo uchokozi na utovu wa sheria wa Beijing kwenye bahari ya South China Sea.

Blinken pia ameelezea vita vya Myanmar kama vyenye kuvunja moyo, wakati akiomba mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya ASEAN, kushirikiana katika kutatua mizozo kama ile ya Gaza na Ukraine pamoja na program ya nyuklia ya Korea Kaskazini. Ingawa Blinken alikosoa China kutokana na matendo yake dhidi ya mshirika wa Marekani Ufilipino kuhusu bahari ya South China Sea, amesifu mataifa yote mawili kutokana kutumia diplomasia, saa chache baada ya Manila kukamilisha upelekaji wa vikosi vyake kwenye eneo hilo la bahari linalodaiwa kumilikiwa na China pia.

Uwepo wa vikosi vya Ufilipino kwenye eneo hilo kwa miaka mingi umegadhabisha China, ambayo imezozana na Ufilipino kutokana na upelekaji wa vikosi kwenye meli ya kijesji kwenye bandari ya Second Thomas Shoal, suala ambalo limeendelea kuzua wasi wasi. Mataifa yote mawili wiki hii yamefikia makubaliano ya namna ya kufanya operesheni zao kwenye eneo hilo.

Blinken pia anafanya mazungumzo na mwenzake wa China Wang Yi, baada ya kikao cha kiusalama na viongozi wa ASEAN ambacho kimekuwa kikifanyika Laos. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na wanadiplomasia wa ngazi za juu kutoka mataifa yenye nguvu kama Russia, Australia, Japan, Uingereza na Umoja wa Ulaya.

Blinken pia amesema kuwa Marekani inajitahidi iwezavyo kuleta sitisho la mapigano huko Gaza, pamoja na kutafuta njia ya amani na usalama wa kudumu.

Source : VOA Swahili

SHARE THIS POST