Anayedaiwa kuchukuliwa na Polisi kwa mahojiano akutwa ameuawa Zanzibar
“Mwanangu ameuawa, kifo cha kikatili naomba haki itendeke waliofanya hivi wachunguzwe, ni kweli kifo kipo lakini sio cha namna hii…” Hii ni kauli ya Saada Ramadhan Mwendwa mama mzazi wa Ramadhan Idd Shaaban (48) akianza kusimulia jinsi mwanaye alivyochukuliwa na watu waliojitambulisha ni askari wakidai wanakwenda kufanya mahojiano naye lakini aliokotwa akiwa amefariki dunia eneo la Mbuzini Kijichi Unguja. Kwa kipindi cha hivi karibuni matukio ya watu kutekwa, kupigwa, kuumizwa na kuuawa yameshika kasi kwa upande wa Tanzania Bara, hata hivyo kwa Zanzibar hayajawahi kusikika. Akizungumza na Mwananchi kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Richard Mchomvu bila kufafanua zaidi amesema wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo na ukikamilika zitatolewa taarifa zaidi. Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi Video na Hamis Mniha