Alexei Navalny aliamini atakufa akiwa gerezani; kulingana na kitabu chake

3 months ago 304

Kumbukumbu  zote zitaadhimishwa bila mimi kuwepo. Sitaweza kamwe kuwaona wajukuu zangu, aliandika Navalyn.

Muasi raia wa Russia Alexei Navalny ambaye alikuwa mpinzani mkuu wa kisiasa wa Rais Vladimir Putin kabla ya kifo chake mwezi Februari aliamini atakufa akiwa gerezani, kulingana na kitabu chake cha kumbukumbu baada ya kifo, ambacho kitatolewa Oktoba 22.

The New Yorker ilichapisha dondoo kutoka kwenye kitabu siku ya Ijumaa, ikielezea maandishi kutoka kwa Navalny aliyoyakusanya kutoka gerezani na awali. “Nitatumia maisha yangu yote gerezani na nitakufa hapa,” aliandika Machi 22, mwaka 2022. Hakutakuwa na mtu yeyote wa kusema kwaheri.

Kumbukumbu zote zitaadhimishwa bila mimi kuwepo. Sitaweza kamwe kuwaona wajukuu zangu”. Navalny alihukumiwa kifungo cha miaka 19 jela kwa mashtaka ya siasa za msimamo mkali katika gereza la Arctic.

Kifo chake kilitokea Februari 16 akiwa na umri wa miaka 47 ambacho kilizua shutuma kubwa, huku wengi wakimlaumu Putin.

Source : VOA Swahili

SHARE THIS POST